Tunapenda kuwajulisha wanachama wote kwamba mchakato wa uchaguzi wa viongozi utafanyika kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na ratiba ya uchaguzi iliyotolewa.
Wanachama wote wenye sifa wanahimizwa kushiriki kikamilifu katika hatua zote za uchaguzi ili kuchagua viongozi watakaowawakilisha kwa uadilifu, uwajibikaji na weledi.
Tafadhali tembelea website hii mara kwa mara kwa taarifa rasmi, ratiba, fomu, vigezo vya wagombea na matangazo mengine muhimu kuhusu mchakato wa uchaguzi.
WANACHAMA MNAHAMASISHWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU ILI KUPATA VIONGOZI BORA WA KULINDA NA KUTETEA MASLAHI YA WAFANYAKAZI “MSHIKAMANO DAIMA”.