Chama cha Wafanyakazi Mashambani na Kilimo Tanzania (TPAWU) siku ya AlhamisiĀ tarehe 09/10/2025 na Ijumaa tarehe 10/10/2025 kilikutana na kufanya mafunzo na kikao cha kiutendaji katika Hotel ya Njuweni Mjini Kibaha.
Aidha Mwenyekiti wa Taifa TPAWU Ndugu Daniel Bariyanka Joachim alipata nafasi ya kufungua pamoja na kuhudhuria mafunzo yaliyotolewa katika semina iyo.
Mafunzo yalikua ni namna ya ufunguaji wa Mashauri kwa njia ya Kidigitali CMA- Online Case Management System, Mafunzo hayo yalitolewa na Mkufunzi Ndugu Kelvin Shayo, lengo ni kuwawezesha Watendaji kuendena na Matakwa ya tume ya usuluhishi na uamuzi.
Pia Mkufunzi ndugu Yahya Msangi alifundisha mada ya Organizing and Recruitment, lengo ni kuwaongezea watendaji ujuzi katika utoaji wa huduma kwa wafanyakazi katika sekta ya kilimo Tanzania.
Pia Watendaji wakiongozwa na katibu Mkuu Ndugu John Vahaye waliweza kufanya kikao cha kiutendaji na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kuweka Maadhimio ya mwaka 2025/2026
Aidha Watendaji wa Kanda na Sehemu walipata nafasi za kuwasilisha mada za kiutendaji, hususani katika kuelezea Uwezo wao, Madhaifu yao, Fursa wanazoziona au walizoziona katika maeneo yao ya kazi, Vitisho au Changamoto na Malengo waliyojiwekea katika kila kanda ili kuweza kuhakikisha Chama kinazidi kukua.