TPAWU imetembelewa na Bi Tina Cornillie Mkurugenzi wa FOS. FOS ni shirika la kibelgium linalohusika na kulinda haki za Binadamu ikiwa ni pamoja na haki za Wafanyakazi.
Katika ziara yake alipata nafasi ya kutembelea Ofisi za TPAWU Makao Makuu ambapo aliweza kukutana na Katibu Mkuu wa TPAWU Ndugu John Vahaye pia alifanya ziara katika Kanda ya Tanga ambapo alipata nafasi ya kukutana na viongozi wa kamati za Wanawake na baadae alitembelea Shamba la Amboni Spinning Mills kujionea namna Wafanyakazi wanavyofanya kazi.
viva #TPAWU viva #FOS